Pages

Monday, May 6, 2013

BABA ASIMULIA ALIVYONUSURIKA KIFO NA MWANAE, ASEMA ALIONA BORA AFE YEYE LAKINI MWANE APONE ALIAMUA KUMKUMBATIA KIFUANI



 Baba akiwa amemkumbatia mtoto wake, Mazazi huyo alisema aliona bora afe yeye lakini mwanae apone.
  Babu akiwa chini huku biblia yake pembeni akishindwa kuamini kilichotokea.Huku kulia Mama akiinua mikono juu kumshukuru mwenyezi Mungu kwa yote yaliyotokea.
 Baadhi ya wanausalama wakiangalia mabaki ya vipande vya bomu lililoripuka jana wakati wa ibada kwenye Kanisa Kuu la Katholiki Jimbo la Arusha.

Livingstone Mkoi na Zakia Shabani Arusha

Wakati nchi ikiwa kwenye mtikisiko mkubwa kufuatia tukio la kusikitisha la kulipuliwa kwa Kanisa huku waumini zaidi ya 60 wakijeruhiwa vibaya pamoja na wawili kupoteza maisha Baba mmoja ambae nae alinusurika kufa na mwanae wa kiume mwenye umri wa miaka mitatu amelezea jinsi alivyomuhurumia mwanae.
Akiongea na mwandishi wetu wa Xdeejayz Jijini humo muda mfupi baada ya tukio hilo Baba huyo aliyejitambulisha kwa jina la Fred Kaaya "45"  alisema kuwa muda wote wa tukio aliomba mungu kumsaidia mwanae asalimikeni heri angepoteza maisha yake kuliko mtoto wake huyo.
Fred aliendelea kusema " Baada ya kusikia kishindo kikubwa kilichoziba masikio yote tukahisi tayari kimenuka hivyo kwa haraka haraka nilimkumbatia mwanangu kifuani huku nikiendelea kumuomba Mungu" Alisema mtu kama anavyoonekana kwenye picha ya kwanza akiwa chini amemkumbatia mtoto wake huyo.

Aidha baada ya tukio hilo  Jijini Dar watanzania mbalimbali walionekana kusikitishwa na tukio  na kusema kuwa sasa tanzania inaelekea kubaya hivyo serikali inatakiwa kufanya juhudi za haraka sana kuinusuru nchi na matukio haya" Jamani hata miezi minne haijapita tumeshuhudia Padri wa Kanisa Katholiki Zanzibar akiuuliwa kinyama kwa kupigwa risasi tena sasa hivi watu wanarushiwa mabomu jamani Serikali mbona haiamkii kuweka tahadhari?" Alisema mwananchi mmoj aliyefahamika kwa jina la Antonie Nyanyembe
Hata hivyo wananchi hao waliendelea kutoa ushauri kwa serikali kupita kupita wizara husika zenye dhamana ya usalama kuweka tahadhari kuliko kusubiri watu wafe ndio waanze kuunda tume ambazo matokeo yake huo hamana chochote.

No comments:

Post a Comment