hk CONTACTS

hk CONTACTS

Thursday, April 18, 2013

SAFARI YA MWISHO YA MAREHEMU FATUMA BINTI BARAKA A.K.A BI KIDUDE


  
Jeneza la bibi likielekea msikiti kwa ajili ya kusaliwa.Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kugharamia mazishi ya Gwigi la Sanaa ndani ya ukanda wa Afrika ya Mashariki na mipaka yake Anti Fatma Binti Baraka (Maarufu Bi. Kidule) aliyefariki dunia jana mchana baada ya kuugua kwa muda mrefu.Balozi Seif akitoa ubani wa shilingi Milioni 2 kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa familia ya marehemu amesema jamii na waswahili wote katika mwambao wa Afrika Mashariki wanafahamu mchango mkubwa wa Msanii Bi. Kidude  katika fani ya muziki wa taarabu.
Mwanamuziki mkongwe, Bi Kidude binti Baraka aliyefariki dunia jana amezikwa leo mchana huko Zanzibar na katika mazishi hayo alihudhuria Mhe. Rais Dr. Ali Mohamed Shein. Pichani ni jeneza la marehemu Kidude likielekea makaburini.
 
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohammed Ali Mohamed Shein, wakishiriki katika dua maalum ya kumswalia marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', iliyofanyika mchana huu katika Msikiti wa Mwembeshauri mjini Zanzibar. Bi Kidude anatarajia kuzikwa mchana huu kijijini kwao Kitumba Wilaya ya Kati, Unguja.
 
Mwili wa marehemu Bi. Kidude ukitolewa msikitini
 

Umati wa watu wakipokezana mwili wa Marehemu Bi. Kidude baada ya kutolewa msikitini ukipelekwa mazishini
 
 Mhe. rais wa zanzibar Dr Shein alipokuwa akiwasili kwenye mazishi hayo.  Ulinzi ulikuwa ni wa kutosha


Mhe. rais wa zanzibar Dr Shein na viongozi wengine wakitoa heshima zao za mwisho mbele ya marehemu Bi Kidue kabla ya kuhifadhiwa kwenye jeneza.
 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika dua ya pamoja kumuombea Gwiji la sanaa Zanzibar Bi. Fatma Binti Baraka (Bi. Kidude) nyumbani kwake Rahaelo nyuma ya Studio ya ZBC Redio.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na baadhi ya Familia ya Bi. Kidude wakati alipofika kutoa mkono wa pole kwa ndugu na jamaa wa msanii huyo. Kushoto kwa Balozi  ni Ndg. Haji Ramadhani Suwed na kulia ni Bw. Abdullrahman Saleh.

  Sehemu ya umati uliohudhuria mazishi hayo upande wa kina mama

Umati mkubwa wa Wananchi walioshiriki mazishi ya Msanii Gwiji wa sanaa kanda ya Afrika Mashariki na Mipaka yake  Bi. Fatma Binti Baraka (Bi Kidude) nyumbani kwake Rahaleo nyuma ya Studio ya ZBC Redio.

Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wakiendelea na dua ya kumuombea msanii Gwiji wa Taarab Bi. Fatma Binti Baraka ( Bi Kidude) nyumbani kwake Rahaleo.
 
Mtangazaji Hassan Bond, Fid Q, Diamond Platnumz na Ruge Mutahaba wakiwa msibani nyumbani kwamarehemu bi Kidude,  Zanzibar


Taratibu za Mazishi zikiendelea.
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania , Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Hapa ndipo alipozikwa Bi. Kidude

No comments:

Post a Comment