Pages

Tuesday, March 12, 2013

TID ACHEZEA KICHAPO CHA KINYAMA




Mwanamuziki nyota wa Bongo flava ambaye kwa sasa amejikita kwenye muziki wa dansi, Khalid Mohammed ‘TID’, wiki iliyopita alionja joto ya jiwe baada ya kudundwa hadi kutolewa nundu puani na mtangazaji wa Clouds TV, Cedou Ayoub a.k.a Babuu.




Tukio hilo la aina yake lililotokea wiki iliyopita kwenye kiota cha burudani Bongo pale Club Maisha na kushuhudiwa na watu kibao ambapo chanzo chake kikidaiwa ni kudaiana hela.



Chanzo chetu kilimwaga umbea kuwa, siku ya tukio hilo TID alikuwa amealikwa kwenye uzinduzi wa albamu ya mwanamuziki Country Boy iliyokuwa inafanyika mjengoni humo, ambapo baada ya onesho hilo kuisha ndipo TID akiwa ‘mitungi’ alimfuata Babuu na kuanza ‘kumzingua’.




Hata hivyo, chanzo chetu kiliendelea kueleza kuwa, baada ya walinzi wa ukumbi huo kuona hali tete ya uvunjifu wa amani waliwasihi watu hao kutoka nje kabisa ya ukumbi, huku mtangazaji huyo akiwaomba walinzi hao wawaache wapimane ubavu kidogo na walipotoka nje wakaachiwa ‘ulingo’ ndipo ngumi zilianza kupigwa.




Habari zaidi toka eneo la tukio zilisema kuwa: “Watu waliwazunguka huku wakishangilia kwa muda wa dakika tano ngumi zinapigwa ndipo maabaunsa wakawaamua, lakini, tayari TID alikuwa ameshatolewa manundu kadhaa puani.”




Aidha, kwa upande wa Babuu, alipotafutwa kupitia simu yake ya kiganjani, iliita bila kupokelewa.



Hata hivyo, watu wa karibu na Babuu walilieleza kuwa, kufuatia TID kuchezea mkong’oto huo, kumezuka ‘bifu’ kubwa na kuna wasiwasi wa kutekana kwa mastaa hao hivyo huku Mkurugenzi wa Clouds Media, Ruge Mutahaba akitakiwa kuingilia kati suala hilo ili kuepusha balaa.

No comments:

Post a Comment