hk CONTACTS

hk CONTACTS

Thursday, February 7, 2013

RICH ONE ATOKA UPYA NA JUMA NATURE

 Yule msanii mkongwe wa tanzania alietokea katika kundi la JOINT MOBB moja kati ya makundi ya mwanzo mwanzo kabisa katika game hili la bongo fleva ambae hivi karibuni alijiunga na kundi la TMK WANAUME FAMILY ametoka upya na ngoma yake kali sana aliyomshirikisha JUMA NATURE NA INSPECTOR HAROUN, Nyimbo hiyo yenye maadhi ya LUMBA  imefanyika katika studio za HALISI RECORDS chini ya producer mahiri Ben mwamba. na mixing kufanyika katka studio za MPO AFRIKA,Uchanganywaji wa maproducer katika nyimbo hii umeleta radha tofauti na tamu sana.

Rich one aliiambia hyperblog kuwa sasa ameamua kurudi kwenye game kwa nguvu zote na kusema kuna watu waengi wanasema wakongwe hawatoi nyimbo nawengine kusema wagongwe wanapotezwa na wasanii wa wapya alikanusha usemi huo kwakusema sio kweli, maana wakongwe wanatoa ngoma mpya lakini saport ni chache sana ukilinganisha nja saport za wasanii wapya hivyo rich one amependekeza kupewa promo ya kweli na wataona mabadiliko makubwa kutoka kwa wasanii wakongwe kama yeye. wimbo wake mpya unaitwa FLANI amemshirikisha juma nature na inspector haroun a.k.a babu.kaa tayari kuwa wa kwanza kusikiliza na kudowload wimbo huo wa FLANI kupitia blog hii ya hyperhk.

No comments:

Post a Comment