Lulu akiwa
anaingia Mahakamani leo january 28 2013 akiwa na shauku ya kupata
dhamana.
Mahakama
kuu leo imetangaza dhamana ya mwigizaji Lulu lakini iwapo atatimiza masharti
aliyopangiwa ambayo ni pamoja na kuwasilisha hati yake ya kusafiria, kutosafiri
nje ya Dar es salaam, kujiwakilisha au kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza
ya kila mwezi pamoja na wadhamini wake wawili ambao kila mmoja adhamini kwa
shilingi milioni 20 za kitanzania.
Upande wa
familia ya Lulu umesema masharti yote yaliyotajwa wanaweza kuyatimiza leo leo
hivyo wanasubiri tu jibu la msajili ambae ndio anatakiwa kuhakikisha hayo
masharti yametimia kisha ruhusa ya kumkabidhi Lulu kwa familia yake
itolewe.
Taarifa za
ndani ni kwamba uwezekano wa Lulu kuachiwa upo kuanzia january 29 2013 ambayo ni
kesho kwa sababu kuna watumishi wawili wa serikali ambao wapo kikazi mkoani
Pwani na ndio walitakiwa kutia saini dhamana ya Lulu wakiwa ni sehemu ya
masharti.
.
.
.
.
Hapa ni
wakati alipocheka sana pale mwandishi mmoja wa kike ambae pia alikua akimpiga
picha alipokua akimlainisha Lulu kwa maneno baada ya mwigizaji huyo kuficha uso
wake alipokua akipigwa picha, alisema alikua anaumizwa macho na mwanga wa
kamera.
.
.
Mama mzazi
wa Lulu ni mwenye nguo nyeupe na nyeusi.
Unaweza
kumsikiliza mwigizaji Dr Cheni hapo chini, ni mmoja ya watu waliokaribu na
familia ya Lulu na ameshirikiana nayo kwa muda mrefu sana kwenye hii kesi
ikiwemo kufatilia mawakili, kushughulikia dhamana na mengineyo
No comments:
Post a Comment