hk CONTACTS

hk CONTACTS

Sunday, May 4, 2014

MASHUJAA BAND YASHUKURU MASHABIKI WAO KWA TUZO WALIZOPATA



 ASANTENI SANA WADAU WETU……TUZO 3 mmetupa moyo tena!
Tulipotoa nyimbo tuliwasmbazia kwenye simu na mitandao ili mzisikie…..tuliwaomba ushauri na tuliwasiliana nanyi mara kwa mara,kazi zetu mlizisifia na mlitoa maoni ambayo tuliyafanyia kazi..ikaja michakato ya tuzo za kili tuliwataarifu tukawaomba mtupigie kura…mara zamu yenu ikafika ya kuamua na mmeshaamua na hatimaye mmetupatia tuzo 3 kwa mwaka huu yaani wimbo bora….rapa bora na bendi bora…Tuna furaha isiyo kifani lakini kikubwa hapa ni shukurani kwenu ninyi kwani mlijitoa mpaka mkatumia pesa zenu kutupigia kura kwani kila kura ilikuwa inalipiwa….Tuna deni kubwa sana kwenu kwani mnatudai sana kazi zilizo bora na tunawaahidi tungo zilizo bora zaidi mwaka huu…asanteni sana na mungu awabariki


No comments:

Post a Comment